|
TANZANET-KANDORO PRIZE [ main
page | Guidelines
| Biographical Note | Award
2002 | Award
2003
]
TANZANET Kandoro-Prize 2002 is awarded to poet Ahmed
Akilimali Snowhite
The TANZANET Kandoro-Prize 2002 is awarded to poet Ahmed
Akilimali Snowhite of Ujiji, Kigoma Tanzania. The prize has
been awarded in recognition of the poet's mastery of Kiswahili
verse and, contribution to the language.
Sheikh Akilimali Snowhite was born 1926 in Ujiji, Kigoma where
he has spent most of his adult life. He has produced an
extensive body of work in newspapers and for the radio. His
epic work ”Diwani ya Akilimali”, Snowhite continues the grand
lineage of 20th Century Kiswahili poetry
narration with a brilliant interweave of panoramic spiritual
information with political-economic chronicle of Tanzanian
society in the 1960s and beginning of 1970s.
His uncompromising distaste for rhetoric and his almost
prosaic frugality in the use of metaphors and reintroduction
of epigrammatic and dramatic modes, updated Kiswahili poetry
for the post-Shaaban Roberts' verse for the
21th Century. These attributes, introduced by
renowned Kiswahili poets Sheikh Amr Abeid and Saadani A.
Kandoro found their true bearer in Akilimali Snowhite. And
like all those bearers of a truly human truly transforming
art, his poetry is deeply impure, deeply defiant and deeply
seeking and absolutely clear that the verse must be truth to
the human condition and beauty. His frank, and brilliantly
alive, tribute to his mother in “Mama” epitomises what makes
Akilimali Snowhite one of the most important poets writing
today.
Kandoro-Prize Committee, on behalf of the TANZANET Community,
awards 2002 Kandoro Prize to Ahmed Akilimali Snowhite.
Dr. Aziz P. Mlima Chairperson-Kandoro Prize Committee, 2002
Tuzo
ya Kandoro mwaka 2002 ametukunikiwa mshairi Sheikh Ahmed Akilimali
"
Snowhite"
Jopo la TANZANET Tuzo ya Kandoro linayofuraha kutangaza tuzo
ya Mwaka 2002 ametukunikiwa mshairi Sheikh Ahmed Akilimali
Snowhite wa Kigoma, Tanzania. Sheikh Akilimali Snowhite
ametunikiwa tuzo la Mwaka 2002 kwa kuzingatia mchango wake
katika ushairi na lugha ya Kiswahili.
Sheikh Ahmed Akilimali Snowhite alizaliwa mwaka 1926
mjini Ujiji, Kigoma ambapo anaishi sasa hivi katika kitongoji
cha Katenyanga. Tangu ujana wake Akilimali Snowhite ameshiriki
katika malumbano ya tenzi. Umahiri wa Akilimali Snowhite
unajidhirisha kutoka katika kitabu chake ”Diwani ya
Akilimali,” ambapo amedurusi masuala mbalimbali, kama upeo wa
uhai wa binaadamu, hisia za kutosadikika na jitahada ya
kupambana na uonevu. Mchango wa Akilimali katika mapambano
dhidi ya utawala wa kigeni, ambapo lugha ni miongoni mwa
silaha muhimu, haukuishia katika tenzi tu bali katika
kushiriki kikamilifu katika masuala ya kugombea uhuru na
heshima ya Mwafrika.
Mbali ya uandishi unatoka katika utamaduni wa tenzi za
Kiswahili, mpangalio wa beti za mistari minne-minne, Akilimali
Snowhite alikuwa ni miongoni mwa washairi wa kwanza kupanua
uwigo wa tenzi hizi kwa kuunganisha beti mbili au tatu pamoja
kuwa shairi moja. Umahiri huu umejitoka katika shairi lake
”Mama” aliloaandika kwa heshima ya kumbukumbu ya mama yeke
mzazi. Miongoni mwa waasisi wa tenzi hizi ni Sheikh Amr Abeid
na Saadani Kandoro.
Kwa kuzingatia mchango huu, wanajopo wa Tuzo ya Kandoro kwa
niaba ya TANZANET, wanamzawadia tunu ya mwaka huu Sheikh Ahmed
Akilimali Snowhite.
Mzee Akilimali aliwahi kuwa mjumbe wa baraza la
Kiswahili sarufi kati ya mwaka 1976 na 1979.
Dr. Aziz P. Mlima Chairperson-Kandoro Prize Committee, 2002
|
Members of the TANZANET-Kandoro Prize Committee
(2002)
Dr. Aziz P. Mlima (Chairperson II (2002-3)
Mr. Yusuf Kalala (Chairperson I (2001)
Mr. Thabit Tambwe (Secretary)
Dr. Balla Maselle (Member)
Ms. Getrude N. Malai (Member) Ms. Saada Al-Ghafry (Member)
Dr. Hassan O. Ali (Member) Mr. Henry Mgaya (Member) Mr.
Richard Madete (Member)
Mailing list: kandoro-prize@tanzanet.org
|
Baadhi ya kazi zake
Mwanadamu Kumbuka
Kufa ni jambo muhimu, kupo kunatusubiri,
Kufa kumetulazimu, kuwa ndani ya kaburi,
Tuvipendavyo vitamu, haviziwii safari,
Mwanadamu kumbuka, siku moja utakufa.
Uhai kwa mwanadamu, siku zote tufikiri,
Kuishi jambo adimu, kwa maisha ya dahari,
Kufa jambo la lazima, hakuna chakustiri,
Mwanadamu kumbuka, siku moja utakufa.
Tupate kila makamu, kila hati ya mfahari,
Si ngao ya kujikimu, bali ni kujiadhiri,
Kufa ni jambo muhimu, mtu hanako hiyari,
Mwanadamu kumbuka, siku moja utakufa.
Kifo kitapo asimu, hakuna alifajiri,
Wafa pasipo salam, na kuyaacha mazuri;
Hutamuaga binadamu, wala humpi habari;
Mwanadamu kumbuka, siku moja utakufa.
Jepesi huwa ni gumu, na neon hulikariri,
Kinywa jufungwa hatamu, usiweze kuashiri,
Hapo ndipo mwanadamu, mwishowe wa machachari,
Mwanadamu kumbuka, siku moja utakufa.
Nguvu ulijikirimu, na cheo cha uayari,
Kikomo hapo hutimu, hubaki watahayari;
Na uendako kuzimu, wangozewa kwa jeuri;
Mwanadamu kumbuka, siku moja utakufa.
Ni misada maalumu, walo hai wadhidiri;
Na wapige baragumu, na kila hali urari,
Pepo hawakukirumu, kama hukutenda heri;
Mwanadamu kumbuka, siku moja utakufa. |